SOKO LA MTANDAO TANZANIA Jisajili na kuweka Matangazo BURE MILELE! 0677775000
classiera loader
image

Ad Details

  • Ad ID: 13685

  • Added: 9th May 2021

  • Sale Price: 3,000

  • Location: Tanzania

  • State: NunuaUza.com

  • Phone: 0677775000

  • Views: 505

Description

JINSI YA KUTENGENEZA KACHORI ZA VIAZI
📍MAHITAJI

➖Viazi (kilo Moja)

➖Kitunguu saumu(thomu) kijiko 1 Cha chakula
➖ Tangawizi Kijiko 1 cha chakula

➖Chumvi ( kijiko kimoja Cha chakula)

➖Pilipili ya kusaga

➖Ndimu 1

➖Mafuta ya kupikia

➖Unga wa dengu au Ngano Kiasi.

📍NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA:

➖Chemsha viazi mpaka viwive, kisha vitoe maganda na uviweka ndani ya bakuli.

➖Vipondeponde kwa mkono mpaka viwe laini.

➖Saga thomu na tangawizi kisha changanya na viazi .

➖Weka chumvi, ndimu na pilipili ya unga kisha uonje, unaweza kuongeza viungo hivi kwa kadri ya mapenzi yako.

➖Tengeneza madonge ya duara uyapange katika tray.

➖Vuruga unga wa dengu au ngano kwa maji uwe mwepesi kidogo.

➖Weka mafuta ya kupikia ndani ya karai na uliweke kwenye moto.

➖Chovya madonge kwenye unga na uyatose kwenye mafuta ya moto. (Uchomaji wake ni kama kuchoma bajia)

➖Wacha kachori zibadilike rangi kuwa ya njano na uzitoe kwenye mafuta.

Weka Kachori kwenye sahani zipoe tayari kwa kuliwa.

Bids

BID Stats : 0  Bids posted on this ad

Let’s Create Your Bid

Only registered user can post offer *

Ad Price

3,000

classiera loader

Related ads

LIST YOUR BUSINESS TODAY!!