3,000

SAMAKI WA MCHUZI WA NAZI

1 of
Previous Next

Ad Details

  • Ad ID: 13522

  • Added: 25th April 2021

  • Sale Price: 3,000

  • Location: Tanzania

  • State: Dar es Salaam Region

  • Phone: 0677775000

  • Views: 278

Description

*SAMAKI WA MCHUZI WA NAZI*

*MAHITAJI*

*•* Nyanya
*•* Pilipili hoho
*•* Vitunguu maji
*•* Vitunguuswaumu
*•* Carrots
*•* Ndimu
*•* Nazi (tui zito)
*•* Chumvi
*•* Samaki
*•* Tangawizi
*.* Bamia

*NOTE:* 👆👆Unaweza kutumia MAHITAJI yako Kwa kiasi unachotaka.

*MATAYARISHO*

➖Andaa viungo – tangawizi, ndimu, vitunguu saumu – menya, kata na ponda kama inawezekana.
➖Osha samaki vizuri kisha mloweke kwenye viungo (chaganya tangawizi,ndimu,vitunguu saumu na chumvi) kwa muda wa saa moja.
➖Andaa viungo vyako mbadala – nyanya,vitunguu,karoti, na pilipili hoho.
➖Tengeneza tui zito la nazi na hifadhi pembeni.
➖Bandika kikaangio, au sufuria jikoni, weka mafuta ya kula na acha yapate moto.
➖Weka samaki. Kaanga samaki ila hakikisha asikauke sana.
Fanya hivyo kwa samaki wote waliobaki.
➖Bandika sufuria jikoni weka mafuta kiasi – unaweza pia kutumia uliyokaangia samaki
Mafuta yakipata moto, weka vitunguu maji kisha koroga hadi kibadilike rangi kiwe rangi ya udongo.
➖Weka kitunguu saumu kisha koroga kidogo kama dakika 1
Weka pilipili hoho na karoti. Koroga kiasi, kwa takribani dakika 2.
➖Weka nyanya na Bamia zako, koroga kiasi ili zichanganyike vizuri.
➖ Funika na mfuniko na acha ziive kwa mvuke.
➖Nyanya zikiiva, weka tui zito liache lichemke kama dakika 10.
➖Mchuzi ukiwa mzito weka samaki na koroga mpaka samaki achanganyikane na viungo vizuri.
➖Acha jikoni kwa dakika takribani 3 nakisha ipua.

tayari Kwa Kuliwa

Bids

BID Stats : 0  Bids posted on this ad

Let’s Create Your Bid

Only registered user can post offer *

Ad Price

3,000

classiera loader