3,000 PRO SERVICES
Ad Details
-
Ad ID: 13519
-
Added: 25th April 2021
-
Sale Price: 3,000
-
Location: Tanzania
-
State: Dar es Salaam Region
-
Phone: 0677775000
-
Views: 535
Description
MAKANDE
🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹
MAHITAJI
1. MAHINDI
2. MAHARAGE
3. KARANGA MBICHI
4. NAZI
5. HOHO
6. CARROT
7. KITUNGUU MAJI
8. CHUMVI
9. CURRY POWDER
10.MAFUTA
11.IRIKI
🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷🌷
JINSI YA KUANDAA
1.Chukua mahindi na maharage na karanga mbichi (karanga sio lazima) vikiwa visafi, andaa jiko lako weka maji ya kutosha ukimaliza weka mchanganyiko wako huo 👆🏽 na funika mpaka viive,
2. andaa nazi yako chuja matui mawili zito na jepesi
3. andaa viungo vyako vyote ☝️
4.weka sufuria jikoni na mafuta kidogo sana, kaanga vitunguu vyako na iriki, vikianza kuwa vya brown weka carrot na hoho (hoho na carrot uache kidogo uje uweke mwishoni pia kwa radha nzuri zaidi), utaweka nyanya kiasi, zikiiva utaweka tomato paste na carry powder na chumvi, koroga alafu weka kande zako, changanya vizuri weka tui jepesi koroga likiiva weka tui zito na hoho na carroti zilizo bakia, koroga mpaka liive, epua tayari kwa kuliwa 😋😋😋
Bids
BID Stats : 0 Bids posted on this ad
Let’s Create Your Bid
Only registered user can post offer *
Ad Price
3,000